JE WAJUA? Nchi ya Saudia Arabia haina hata mto unaopitisha maji? na je wajua? kuna dhahabu mara 200 zaidi ndani ya bahari duniani zaidi ya iliyokuwa imechimbwa hadi sasa ulimwenguni kote?
Siku kama ya leo miaka 18 iliyopita yaani mwaka 1998 Akashi-Kaikyo daraja linaloning'inia yaani (sunspension bridge)na refu kuliko yote duniani lafunguliwa huko Japan
Siku kama ya leo miaka 431 iliyoyopita yaani 5 Aprili 1585, yalifanyika mauaji ya halaiki katika mji wa Harlem nchini Uholanzi, ambacho kilikuwa kitovu cha wapigania uhuru nchini humo. Mauaji hayo yalifanyika kwa amri ya Mfalme wa Uhispania. Jumla ya watu elfu sita wanaaminika kuwa waliuawa kwenye shambulio hilo. Hatimaye Uholanzi ilijipatia uhuru kutoka kwa mkoloni Uhispania hapo mwaka 1609.
Tarehe 5 Aprili 222 iliyopita, aliuawa Georges Danton mmoja kati ya viongozi wa mapinduzi ya Ufaransa. Danton licha ya kusomea taaluma ya sheria, alikuwa mhamasishaji mzuri katika kipindi cha mapinduzi ya Ufaransa. Danton alikuwa akiamini kuwa, sanjari na kuzuia machafuko na maafa ya kibinadamu, utawala wa kifalme nchini Ufaransa ulipaswa kutokomezwa. Amma Robes Pierre mmoja kati ya vinara wakubwa wa mapinduzi ya Ufaransa ambaye pia alikuwa mshindani wa Danton alichukua uamuzi wa kimtia mbaroni Danton na hatimaye kumuuwa.
0 Comments