Kama una tabia ya kujibana kona alafu unajisaidia haja ndogo, mambo yanaweza kukuharibikia kona yoyote !!
Nasubiri kuona hii kitu kwa hamu sana, itapunguza matangazo yaliyoandikwa ‘USIJISAIDIE HAPA, UKIKAMATWA FAINI ….‘
Hii stori nimeipata kwenye ukurasa wa BBCmtandaoni, wamesema Uingereza wako kwenye majaribio ya rangi maalum ambayo haipatani na mkojo kabisa, ikitokea mtu kajibana kujisaidia kwenye ukuta wenye rangi hiyo basi mkojo wote unamrudia mwenyewe !!
London ndio hivyo wameshaamua, na kilichowakasirisha zaidi ni kwamba wamekuwa wakitumia karibu pound 100,000 (kama Tshs. Milioni 318) kwa ajili ya kusafisha kuta ambazo zimekojolewa pamoja na mikojo iliyotuama barabarani, dawa inakuja aisee..
Hapa nina kipande cha video kutoka Ujerumani, miezi 9 iliyopita nao waliwahi kuamua kupaka rangi hiyo kukomesha walevi na wapita njia mabingwa wa kujisaidia kwenye kuta za mitaani.
0 Comments